Saa 1 usiku Yanga itakuwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa kuikabili Namungo Fc katika mchezo muhimu wa kukamilisha mechi 15 za duru ya kwanza
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa leo watashuka uwanja wa Namungo wakivalia uzi wao wa bahati, walioutumia kule Tunisia katika mchezo dhidi ya Club Africain
"Na leo tena… Made From Tunisia Pira PopCorn. Kumbe ndio maana FiFa wamesimamisha World Cup leo ili Dunia ipate burudani ya Wananchi," aliandika Kamwe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Utakuwa mchezo wa saba kuzikutanisha Yanga na Namungo Fc kwenye ligi, mechi tano zikitoa matokeo ya sare na Yanga kushinda mechi moja msimu uliopita
ADVERTISE HERE