Kikosi cha Yanga leo majira ya saa 1 usiku watashuka uwanja wa Majaliwa, Ruangwa kuwakabili Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Huu ni mchezo wa kukamilisha duru ya kwanza, Yanga ikihitaji ushindi ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi
Yanga imejihakikishia kumaliza kwenye nafasi ya kwanza baada ya mechi 15 za duru ya kwanza, ushindi leo utawafanya waendelee kuongeza tofauti ya alama dhidi ya wapinzani wake Azam Fc na Simba katika mbio za ubingwa
Kocha Nasreddine Nabi na vijana wake walipata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Majaliwa jana usiku, ambapo kocha msaidizi Cedric Kaze alisifu ubora wa uwanja huo akiamini leo watakuwa na mechi nzuri


ADVERTISE HERE