Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amewaita mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Majaliwa leo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc
Yanga watakuwa wageni wa Namungo katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku
Kaze amesema mechi hiyo itahitimisha duru ya kwanza hivyo wanawahitaji mashabiki kuja kwa wingi kuwashangilia
"Tunakwenda kucheza katika uwanja mzuri wa Majaliwa ambao haujatumika sana, hivyo tunaamini tutakuwa na mchezo mzuri. Ni mechi ya kufunga raundi ya kwanza ya ligi, hivyo tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi ili tufunge vizuri raundi hii," alisema Kaze
Akizungumzia maandalizi ya mchezo Kaze amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo na habari njema ni kurejea kwa baadhi ya wachezaji waliokosa mechi iliyopita
"Mchezo uliopita tuliwakosa wachezaji kadhaa akiwemo Fiston Mayele, Dickson Job, Jesus Moloko na wengine lakini wamerejea mazoezini na tunaamini watatusaidia"
Kikosi cha Yanga kilitua Ruangwa mapema jana wakitokea Mtwara ambapo waliweka kambi ya siku moja kujiandaa na mchezo huo