Mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari amesema wanatambua mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Namungo Fc utakuwa mgumu lakini wako tayari kuzipigania alama tatu
Kikosi cha Yanga kimeweka kambi ya muda mfupi Mtwara ambapo jioni ya leo watafanya mazoezi mkoani humo kabla ya safari ya Ruangwa
Kibwana amesema ratiba imekuwa changamoto kwao lakini wanapambana
"Ratiba ni ngumu kidogo, tumacheza jana, leo tumesafiri na Jumatano tunacheza na Namungo Fc. Ligi ni ngumu, ushindani umekuwa mkali hivyo kila mchezo kwetu ni kama fainali," alisema Kibwana
Kibwana alikuwa sehemu ya kikosi kilichopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons jana ambapo baadae alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Djuma Shabani
Ni mmoja wa wachezaji katika kikosi cha Yanga ambao wamecheza dakika nyingi msimu huu