Kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumapili, Disemba 04 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, baadhi ya wachezaji waliokosekana katika michezo iliyopita kutokana na sababu mbalimbali, wamerejea
Djuma Shaban, Farid Mussa na Feisal Salum 'Fei Toto' wamerejea kikosini baada ya kumaliza changamoto zilizokuwa zikiwakabili
Kulingana na taarifa ya Yanga, Farid amerejea baada ya kumaliza matatizo ya kifamilia. Nyota huyo alikuwa na ruhusa kutoka kwa uongozi
Djuma alikuwa akisumbuliwa na tatizo la nyama za paja, daktari wa Yanga amethibitisha kuwa nyota huyo yuko tayari kurejea kikosini


Feisal alipata majeraha ya kifundo cha mguu ambayo aliyapata wakati Yanga ikichuana na Dodoma Jiji
Yanga inaendelea na mazoezi Avic Town kujiandaa kuwakabili Tanzania Prisons katika mchezo ambao Wananchi wanazihitaji alama zote tatu