Mshambuliaji Yacouba Songne yuko tayari kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani mwaka mmoja
Yacouba sasa yuko fiti kwa asilimia 100 akiwa na ari kurejea kuitumikia Yanga pale dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameonyesha kuwa na imani kubwa na mshambuliaji huyo na ndio maana alipendekeza abaki licha ya mkataba wake kumalizika
Yanga italazimika kuacha mchezaji mmoja wa kigeni ili kumsajili Yacouba dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa Disemba 15
Kabla ya kuumia mwezi Novemba 2021, Yacouba alikuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha kocha Nabi
Yacouba anaweza kutumika kama mshambuliaji wa kati au winga
ADVERTISE HERE