FT : St Louis 1-1 Yanga, agg(1-2)

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2018
FT : St Louis 1-1 Yanga, agg(1-2)
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wamesonga mbele raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya St Louis katika mchezo wa marudiano uliopigwa dimba la Stade Linite, Victoria Shelisheli.

Yanga imefuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 kufuatia kushinda bao 1-0 katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza.

Bao la Yanga lilipatikana kwenye dakika ya 45 mfungaji akiwa Ibrahim Ajib aliyeunganisha vyema krosi ya chinichini iliyochongwa na Hassani Kessy.

Kabla ya kuingia kwa bao hilo, Yanga ilikosa nafasi kadhaa za wazi.

Kipindi cha pili wenyeji walikuja juu kutafuta bao la kusawazisha na walifanikiwa kulipata kwenye dakika za majeruhi.

Hata hivyo bao hilo halikuweza kuizuia Yanga iliyosonga mbele kwa ushindi wa jumla kwani St Louis walitakiwa kufunga mabao matatu kufanikiwa kufuzu.

Kwenye mchezo wa leo, Kocha George Lwandamina alifanikiwa kimbinu kwani Yanga ilitawala vyema sehemu ya kiungo ikiwa na viungo watano.

Hata hivyo kwenye kipindi cha pili Yanga ilipata pigo pale kiungo wake Said Juma Makapu alipoumia na kushindwa kuendelea na mchezo.

Nafasi yake ilichukuliwa na Raphael Daudi ambaye alimanusura aifungie Yanga bao la pili kama si shuti lake kupaa langoni kwa St Louis.

Yanga sasa inasubiri mshindi kati ya El Marreikh vs Township Rollers ya Botswana kwa ajili ya hatua inayofuata.

Habari njema zaidi ni kwamba Yanga inacheza na tiketi mbili mkononi kwani iwapo itafanikiwa kumtoa mpinzani wake anayefuata itatinga hatua ya makundi lakini kama itashindwa basi itacheza raundi ya pili michuano ya Shirikisho inayoshiriki klabu ya Simba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’