Mechi nane, ndani ya mwezi sio rahisi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Nov 2022
Mechi nane, ndani ya mwezi sio rahisi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewapongeza Ihefu Fc kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga

Nabi amesema Ihefu walicheza vizuri na walistahili ushindi mbele ya wachezaji wake ambao walionyesha kuchoka

Nabi amesema sio rahisi kwa mchezaji kucheza mechi nane ndani ya mwezi mmoja, ikiambana na safari za kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine

Aidha Nabi amesema kupoteza mchezo huo kutawaondolea presha ya unbeaten na wana muda wa ku-recover katika mbio za ubingwa

"Nawapongeza Ihefu Fc kwa ushindi, walikuwa bora uwanjani na nidhamu yao ilikuwa nzuri. Hatukucheza vizuri. Nidhamu yetu ya mchezo haikuwa nzuri na miili ya wachezaji ina fatigue kubwa . Kuna wakati walikuwa hata wazito kukimbia"

"Ratiba imekuwa ngumu sana kiasi cha kuchosha wachezaji. Tumecheza takribani mechi 8 ndani ya mwezi mmoja na tuna safiri sana. Muda mwingi ni mazoezi basics na si ya kujenga miili na mifumo kutokana na muda"

"Wakati mwingine ni vyema kupoteza mechi baada ya kutofungwa kwa muda mrefu ili kuirudisha akili katika mfumo wa upambanaji. Kutofungwa muda mrefu pia huchangia kuleta pressure, ni vyema tumepoteza mechi bado mapema hivyo tutafanyia kazi makosa yetu na tutarudi upya uwanjani kwa kasi kubwa," alisema Nabi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’