Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeangazia rekodi ya mechi 49 ambayo Yanga wameweka pasipo kupoteza mchezo kwenye ligi kuu ya Tanzania
Kupitia BBC Swahili, wamebainisha kuwa Yanga imeingia kwenye rekodi ambayo iliwahi kuwekwa na Arsenal katika ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2003/04
"Rekodi kama hii imewahi kuwekwa na Klabu ya Arsenal katika msimu wa 2003/04 ambapo walicheza mechi 49 na kushinda michezo 24 tu na kuacha kumbukumbu za mashabiki wa soka ulimwenguni haswa wale wa Ligi Kuu ya England (EPL)"
"Aidha, rekodi hii haijawahi kufikiwa na klabu nyingine yoyote kwenye historia ya soka katika nchi hiyo Mwanachama wa Afrika Mashariki," ilibainisha BBC
Hii ni rekodi ya aina yake na kwa hakika, huenda ikachukua miaka mingi sana kuja kuvunjwa
Pale Uingereza rekodi ya mechi 49 mpaka leo bado haijaweza kuvunjwa licha ya ubora wa timu kama Manchester City, Liverpool na hata Arsenal wenyewe ambao tayari wamepoteza mchezo msimu huu