Nafasi mbili muhimu usajili dirisha dogo

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
28 Nov 2022
Nafasi mbili muhimu usajili dirisha dogo

Ni takribani wiki mbili na siku kadhaa zimesalia kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa

Katika dirisha hili klabu za ligi kuu zitakuwa na nafasi ya kufanya maboresho ya vikosi vyao kuelekea duru ya pili ya lala salama

Kwa Yanga ni usajili ambao utaweza kuimarisha kikosi kuelekea michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi ambayo droo yake itafanyika Disemba 12 nchini Misri

Yanga imeendelea kuimarika siku hadi siku wachezaji walioongezwa katika usajili wa dirisha lililopita wakianza kuonyesha makali yao

Ni wazi kwenye dirisha dogo kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi hatakuwa na mahitaji makubwa ya maboresho kwani jeshi lake limekamilika kwa asilimia 90. Pengine ni wachezaji wawili tu ambao Nabi atawahitaji kwenye dirisha dogo

Kwanza ni nafasi ya mlinzi wa kati mwenye uzoefu wa michuano ya Kimataifa. Yanga imepania kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Shirikisho, hivyo itahitaji beki mahiri zaidi ya hawa waliopo ili kuongeza ubora katika eneo hilo

Pili Yanga inahitaji mshambuliaji mwenye sifa sawa au zaidi ya Fiston Mayele ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji

Kwa sasa Mayele amekuwa na mzigo mkubwa kwani amekosa ushindani kutoka kwa Heritier Makambo ambaye ni majeruhi

Nabi alilazimika kumjumuisha kikosini kinda Clement Mzize ambaye anasaidiana na Mayele katika eneo la ushambuliaji

Nje ya maboresho hayo, Wananchi wana timu imara ambayo pasipo na shaka inakwenda kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo

Maboresho watakayofanya yatakuwa maalum zaidi kwa ajili ya michuano ya kombe la Shirikisho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’