Kwa sasa unapozungumzia ubora wa kikosi cha Yanga hutakosa kuwataja wachezaji wawili kutoka DR Congo, mlinzi wa kushoto Joyce Lomalisa na winga Jesus Ducapel Moloko
Wachezaji hawa wamekuwa na mchango mkubwa kwenye ushindi wa Yanga katika mechi za hivi karibuni
Nakumbuka mwanzoni mwa msimu wote walikuwa kwenye wakati mgumu mbele ya mashabiki lakini kwa sasa ni kama wamepindua meza
Moloko ndiye kinara wa kutoa pasi za mabao kwenye kikosi cha Yanga akiwa na assist 3 wakati Lomalisa nae akiwa na assist 2
Lomalisa ametuliza presha ya Wananchi kwani sasa wanajua wana mtu wa kazi kwenye safu ya ulinzi upande wa kushoto

ADVERTISE HERE