Mara kwa mara utasikia mijadala kuwafananisha washambuliaji mbalimbali wa soka duniani
Hata hapa Tanzania mijadala hiyo ipo, Fiston Mayele ameshindanishwa na wengi lakini takwimu zake siku zote zimesimama kumtetea
Ukizungumzia mshambuliaji aliyepata mafanikio zaidi msimu huu Tanzania, Mayele anaongoza
Mayele ana wastani wa kufunga bao katika kila mechi, kwani katika mechi 17 alizocheza katika mashindano yote, amefunga mabao 17
Mabao 8 ligi kuu, mabao 7 ligi ya mabingwa na mabao mawili Ngao ya Jamii

ADVERTISE HERE