Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amemaliza adhabu ya kukosa mechi tatu sasa akiwa tayari kurejea kikosini kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi
Aziz Ki ambaye alipewa ruhusa kwenda kuitumikia timu ya Taifa, alikosa mechi dhidi ya Kagera Sugar, Singida Big Stars na Dodoma Jiji
Fundi huyo mwenye mabao mawili katika ligi kuu ya NBC msimu huu, mlinda kango Djigui Diarra na Gael Bigirimana wamerejea kutoka kwenye majukumu ya timu za Taifa
Bigirimana alikuwa sehemu ya wachezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa mkoani Singida juzi
Nae kiraka Yannick Bangala anarejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kadi tatu za njano
Bangala alikosa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji
