Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewapongeza wachezaji kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Liti, mkoani Singida
Nabi amesema haukuwa mchezo mwepesi kwani walikabiliana na timu yenye matumizi makubwa ya nguvu uwanjani. Hata hivyo vijana wake walipambana na kufanikiwa kupata ushindi huo muhimu
Nabi ameutoa ushindi huo zawadi wa mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao kwenye uwanja wa Liti
"Ushindi huu ni zawadi ya wachezaji kwa mashabiki wetu. Tulicheza dhidi ya timu inayotumia nguvu sana lakini wachezaji wamejitoa mno, najivunia kundi hili la wachezaji nilionao," alisema Nabi
Baada ya ushindi huo, Yanga inarejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo unaofuata ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa