Wananchi wako mkoani Singida ambapo jioni ya leo watashuka katika uwanja wa Liti kuwakabili Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Ni mechi nyingine muhimu kwa Yanga kushinda ili kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi
Kocha Nasreddine Nabi na vijana wake wamepata siku mbili za kufanya mazoezi mkoani Singida ambapo jana jioni walikamilisha maandalizi yao katika uwanja wa Liti
Nabi alisifu ubora wa uwanja huo hivyo leo mashabiki wa Yanga watarajie burudani ya aina yake kutoka kwa timu yao
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema leo wataendeleza utaratibu wao wa kusimama kumpongeza kocha Nabi, benchi la ufundi na wachezaji kwa kucheza mechi mfululizo pasipo kupoteza
Leo tukio litafanyika dakika ya 47, tukio hilo pia litatumika kumpongeza Mfadhili/Mdhamini wa Yanga Ghalib Said Mohamed (GSM) ambaye majuzi ilikuwa kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa