Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa mshambuliaji Heritier Makambo atakuwa nje kwa takribani wiki sita kuuguza jeraha la kifundo cha mguu
Taarifa ya kitabibu imebainisha kuwa Makambo amevunjika mfupa mdogo wa kifundo cha mguu ambapo matibabu yake yatachukua wiki sita kuweza kupona kabisa
Hii ina maana kwa sasa Yanga inamtegemea mshambuliaji mmoja Fiston Mayele pamoja na kinda Clement Mzize aliye pandishwa kutoka timu ya vijana
Ni wazi, Yanga italazimika kuongeza mshambuliaji katika usajili wa dirisha dogo litakalofunguliwa Disemba 15
ADVERTISE HERE