Wananchi leo wanarejea uwanja wa Benjamin Mkapa kupepetana na Singida Big Stars katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC
Yanga itashuka dimbani ikiwa na dhamira moja tu, kushinda mchezo huo na kurudi juu katika msimamo wa ligi
Baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao ulipigwa uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na Wananchi kuibuka na ushindi wa bao 1-0, kikosi kilirejea Dar na wachezaji kupewa mapumziko ya siku mbili
Ni baada ya kucheza mechi nne ndani ya siku 11, mapumziko hayo yamewarejesha wachezaji katika ari nzuri ya kupambana
Katika mchezo wa leo Yanga itamkosa mlinda lango Djigui Diarra aliyesafiri Mali kwa ajli ya majukumu ya timu ya Taifa
Stephane Aziz Ki na Gael Bigirimana nao watakosekana pia wakiwa kwenye majukumu ya timu za Taifa ingawa kwa upande wa Aziz Ki, pia anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, leo atakosa mechi ya pili
Ni mechi kubwa ambayo itaambatana na burudani ya soka kwani Singida Big Stars inayonolewa na Hans van Pluijm ina wachezaji wazuri ambao hupendelea kuweka soka chini
Ni saa 1 usiku palepale Lupaso..!