Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kaze amesema wanafahamu wanakwenda kucheza na timu yenye wachezaji na kocha mzoefu na mechi za ligi kuu na wamekuwa na mwenendo mzuri msimu msimu huu
Hata hivyo wao watakuwa wakirejea katika uwanja wa nyumbani wakiwa na dhamira ya kushinda mchezo huo
"Sisi tuko tayari kwa mchezo, tunafahamu Singida Big Stars ni tumu nzuri, ina wachezaji wenye uzoefu wa ligi, wachezaji wazuri wanaoweza kuamua mechi na wana kocha ambaye amewahi kuifundisha Yanga"
"Tutawaheshimu Singida Big Stars lakini tumejipanga kupata ushindi. Ukiwa na malengo ya kuwa bingwa unapaswa kushinda mechi kubwa, mchezo huu utakuwa kipimo kizuri kwetu katika mpango wetu wa kutetea ubingwa," alisema Kaze
Kaze amesema Yanga itawakosa baadhi ya wachezaji ambao wameitwa timu za Taifa
"Stephane Aziz Ki atakosekana katika mechi ya pili, yeye amefungiwa mechi tatu na pia tulimruhusu kwenda kwenye majukumu ya timu ya Taifa"
"Wengine ambao wameenda timu za Taifa ni Djigui Diarra aliyekwenda Mali na Gael Bigirimana aliyekwenda Burundi"
Yanga itakamilisha mazoezi ya mwisho leo tayari kuwakabili Singida Big Stars hapo kesho