Ni suala la muda tu Mayele kutetema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Nov 2022
Ni suala la muda tu Mayele kutetema

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele kesho Alhamisi anatarajiwa kuwaongoza Wananchi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars. Mchezo huo utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 1 usiku

Mayele amecheza mechi tano za ligi pasipo kufunga, lakini ni suala la muda tu pengine 'atatetema' katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars hapo kesho

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema Mayele ni mshambuliaji bora na ataendelea kumtumia kwani hata asipofunga mchango wake katika timu ni mkubwa

"Mayele ni mchezaji mzuri na mkubwa anapitia wakati mgumu tu kwa sasa ambayo ni wachezaji wengi wakubwa wanaupitia bado ananafasi ya kufanya vizuri nitaendelea kumtumia kwenye mechi zilizo mbele yetu"

"Alikuwa ni mfungaji bora katika timu yetu msimu uliopita uwepo wake tu uwanjani unaongeza nguvu na pamoja na kutokufunga amekuwa bora kwenye majukumu ambayo nimekuwa nikimpa ayafanye ni suala la muda atafunga na atarudi kwenye ubora ambao amekuwa akiuonyesha tangu ametua Tanzania," alisema Nabi

Kwenye ligi kuu msimu huu Mayele amefunga mabao matatu akizifunga Polisi Tanzania, Coastal Union na Mtibwa Sugar

Alifunga mabao saba kwenye mechi za mtoano ligi ya mabingwa na alipachika mabao mawili kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba hivyo kumfanya awe amefunga mabao 12 katika mshindano yote mpaka sasa msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’