Jana Jumatatu jioni kikosi cha Yanga kiliendelea kujifua katika dimba la STADE LINITE kujiandaa na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya wenyeji wao St Louis.
Uwanja huo ndio utakaotumika katika mchezo huo ambao utapigwa kesho Jumatano, February 21.
Katika mazoezi hayo ya jioni, kocha wa Yanga George Lwandamina ameendelea kuiongezea makali safu yake ya ushambuliaji kuhakikisha inatumia ipasavyo nafasi itakazotengeneza kwenye mchezo huo.
Matokeo ya ushindi au sare ndio yanayohitajiwa na Yanga kuiwezesha kusonga mbele hatua ya kwanza.
Iwapo Yanga itatinga hatua ya kwanza ya michuano hiyo, itakuwa imejihakikishia kushiriki michuano ya kombe la shirikisho iwapo itatolewa katika hatua hiyo.
Na kama itafuzu hatua ya kwanza (itaivaa Rollers au El Marreikh) basi itatinga moja kwa moja hatua ya makundi

ADVERTISE HERE