Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika moja ya mechi ngumu ambazo Yanga wamecheza msimu huu
Kaze amesema Yanga haikuwa na mazingira bora kuelekea mchezo huo lakini wachezaji wamecheza 'kibingwa' na kuweza kupata matoke
"Mechi ya tisa ya ligi, pointi tatu muhimu sana, siku nne tokea mechi ya kufuzu kombe la shirikisho Afrika. Mechi ya nne ndani ya siku 11 zenye safari nyingi lakini Wachezaji wameonyesha mapenzi na kujitoa kwa ajili ya klabu na mashabiki
"Tupumzike kesho (leo) tujipange kwa mechi inayofuata tarehe 17 Nov dhidi ya Singida Big Stars, itakuwa mechi ngumu sana. Pongezi kwa Wachezaji wameonyesha hali ya kupambana kwenye mazingira magumu sana na mchoko mwingi," alisema