Yanga yaweka kambi pembezoni ya Mji kukwepa 'mitihani'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Feb 2018
Yanga yaweka kambi pembezoni ya Mji kukwepa 'mitihani'
Yanga ipo katika mazingira salama kuelekea mchezo wao dhidi ya St. Louis, keshokutwa lakini maisha waliyokutana nayo katika mji wa Victoria, Shelisheli yamegeuka gumzo kwa msafara wake uliotua jana jioni.

Uongozi wa Yanga uliamua kuiweka timu hiyo pembezoni mwa mji kwani ingekuwa kinyume huenda hali ya utulivu kwa wachezaji kuelekea mchezo huo ingekuwa ndogo.

Asilimia kubwa ya maeneo ya katikati ya Mji Mkuu wa Shelisheli, Victoria ambako Yanga imepakwepa imekuwa na sehemu nyingi za starehe hasa zikichagizwa na idadi kubwa ya watalii ambao wamekuwa wakimiminika visiwani humo kila wakati.

Tofauti na nyumbani Tanzania ambako ni nadra kuona watu wakijazana kwenye kumbi za starehe katika kipindi ambacho sio mwisho wa wiki, kwa Shelisheli wao kila wakati wanautumia kufanya starehe.

Wakati suala la kujisitiri miili likipigiwa kelele kwa kiasi kikubwa nyumbani Tanzania, Shelisheli ni kinyume kwani asilimia kubwa ya wakazi wake wamekuwa wakivaa nusu utupu.

Wanawake wa Shelisheli ambao ni warembo kimuonekano ndio vinara wa kuacha wazi miili yao hata wanavyokuwa kwenye shughuli zao za kawaida na linaonekana sio jambo la kushangaza kwao.

Ni vigumu kukutana na raia wa Sheliaheli akiwa amevaa mavazi yanayofunika mwili mzima tofauti na Tanzania ambako jamii yake inazingatia vilivyo maadili katika uvaaji.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’