Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema ratiba imekuwa sio rafiki kwao wakikosa muda wa kupumzika
Nabi amesema tangu Jumatano Yanga haijafanya mazoezi na kesho wanapaswa kucheza mechi ya ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar
Nabi amesema walikwenda Tunisia kuiwakilisha Tanzania hivyo ni vyema wenye mamlaka ya usimamizi wa soka wakazingatia afya za wachezaji
"Ratiba yetu ni ngumu sana. Tumemaliza muda mwingi kwenye ndege kuliko uwanja wa mazoezi. Tangu Jumatano hatujafanya mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar"
"Tumefika Mwanza jana 7 usiku na tuna siku moja tu ya mazoezi. Hii sio rafiki kwa afya ya mwili wa wachezaji"
"Hatuko hapa kulalamika lakini tunaamini viongozi wa mpira wetu jambo hili kwa wakati mwingine wanatakiwa kulitazama kwa jicho tofauti. Tulikwenda Tunisia kuiwakilisha Tanzania," alisema Nabi