Kikosi cha Yanga kimerejea salama jijini Dar es salaam wakitokea Tunisia ambako walifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Ulikuwa ushinda wa kibabe ugenini wakiwalaza Club Africain bao 1-0 na kutinga makundi kwa matokeo hayo baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Sasa wamerejea nyumbani kuendeleza ubabe wao kwenye ligi kuu ya NBC, baadae watakwea pipa kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa uwanja wa CCM Kirumba Jumapili Novemba 13




ADVERTISE HERE