Ajib, Tshishimbi kuibeba Yanga Shelisheli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Feb 2018
Ajib, Tshishimbi kuibeba Yanga Shelisheli
Mlinda lango Youthe Rostand na Papi Tshishimbi ndio wachezaji pekee wa Kimataifa walio kwenye kikosi cha Yanga nchini Shelisheli kinachojiandaa kuivaa St Louis kwenye mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika.

Rostand amerejea kutoka kwenye majeruhi hivi karibuni hivyo huenda kinda Ramadhani Kabwili akaendelea kulinda lango. Lakini Tshishimbi ana uhakika wa kuwemo kwenye kikosi kitakachoivaa St Louis.

Matumaini ya WanaYanga wengi yako mikononi mwa Tshishimbi, kiungo huyu amekuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya kikosi cha Yanga.

Katika mechi za hivi karibuni, Tshishimbi amefanikisha kupatikana kwa ushindi katika mazingira yasiyotarajiwa.

Bila shaka ataendelea kuifanya kazi hiyo kwenye mchezo dhidi ya St Louis.

Yeye pamoja na mshambuliaji Ibrahim Ajib wamepewa jukumu maalumu la kuhakikisha wanatengeneza nafasi za mabao za kutosha pia kufunga.

Tshishimbi ameifungia Yanga mabao matatu katika ligi kuu ya vodacom huku Ibrahim Ajib akiwa na mabao matano.

Yanga imekwenda Shelisheli ikiwa na mshambuliaji mmoja tu wa asili, Matheo Antony ambaye hata hivyo amekuwa hapati nafasi mara kwa mara.

Hivyo huenda Yanga ikatumia washambuliaji wake wa pembeni katika nafasi ya ushambuliaji wa kati sasa kufanya jukumu la kufunga kuwa la kila mchezaji.

Juma Mahadhi au Pius Buswita ndio wanatarajiwa kuwa washambuliaji wa kati huku Ajib na Tshishimbi wakikabidhiwa majukumu ya viungo washambuliaji.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’