Kwa mara nyingine Stephane Aziz Ki ameipa Yanga ushindi muhimu dhidi ya Club Africain na kukata tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika
Aziz Ki amedhihirisha kuwa mchezaji wa mechi kubwa, licha ya ukosoaji mwingi kutoka kwa wachambuzi, Aziz Ki ameendelea kuwanyamazisha kwa vitendo
Yanga walimsajili Aziz Ki sio kwa ajili ya kuwafurahisha wachambuzi, bali kuisaidia Yanga kupata matokeo katika mechi kama hizi
Kwa ujumla vijana wa kocha Nasreddine Nabi leo walikuwa bora sana licha ya kuwa ugenini
Wachezaji wote wamepambana na wamefanya kile ambacho mashabiki wao walitamani kukiona
Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza, wachezaji walibezwa, walitukanwa, walidharauliwa na kila aina ya kejeli
Lakini jambo la uhakika Wananchi watakwenda kuwapokea JNIA wakirejea wakiwa mashujaa
Droo ya makundi itafanyika Novemba 16 jijini Cairo, Misri Yanga ikiwa miongoni mwa timu 16 zilizofuzu hatua hiyo.!