Yanga imejipanga kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ambao utapigwa kesho Jumatano huko Tunisia
Wananchi wamejichimbia katika Hotel ya nyota tano, Golden Carthage ndani ya Jiji la Tunis hali ya utulivu ikitamalaki na pia ulinzi ukiwa ni mkali
Tangu walipotua Tunis hapo jana wakitokea Sousse, hakuna mchezaji wala kiongozi aliyetoka nje ya Hotel hiyo
Mahitaji yote yanapatikana humo, muda ambao watatoka ni leo saa 12 jioni kwa saa za Tunisia na wataelekea uwanjani kukamilisha mazoezi ya mwisho ambayo yatafanyika katika uwanja wa Hammedi Agrebi Olympic ambao utatumika siku ya kesho
Yanga wamepata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja huo ambao Kipanga Fc waliwekewa ngumu kuutumia wakipewa uwanja mwingine tofauti
Aidha viongozi wa Yanga wamekumbushwa kuhakikisha wachezaji wanakuwa na viatu vizuri kuepuka kuteleza kwani Waarabu 'wataupiga maji ya kutosha' muda mfupi kabla ya mchezo siku ya kesho