Msafara wa kikosi cha Yanga umerejea jijini Tunis tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ambao utapigwa siku ya Jumatano
Yanga iliweka kambi ya ya muda mfupi katika mji wa Sousse nje kidogo ya jiji la Tunis ambako ndipo yalipo makazi ya Club Africain
Mabingwa hao wa nchi wamefikia katika Hotel maarufu ya nyota tano Golden Tulip na wataendelea kubaki hotelini hapo mpaka jioni ya kesho Jumanne, majira ya saa 12 watakapoelekea uwanja wa Olympique Hamadi Agrebi kwa ajili ya mazoezi ya mwisho
Mchezo dhidi ya Club Africain utapigwa katika uwanja huo, Jumatano saa 11 jioni kwa saa za Tunisia (saa 1 Tanzania)

ADVERTISE HERE