Baada ya kukamilisha siku mbili za maandalizi katika mji wa Sousse, jioni ya leo kikosi cha Yanga kitaelekea Tunis yalipo Makao ya Club African tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho ambao utapigwa siku ya Jumatano
Wachezaji wa Yanga wamepata muda mzuri wa mazoezi yenye utulivu hapo Sousse
Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amesema wamekuwa wakati mzuri wa kujiandaa na mchezo huo na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri
Kesho jioni Yanga itakamilisha maandalizi yake kwenye uwanja wa Hammedi Agrebi Olympic ambao utatumika siku ya Jumatano
ADVERTISE HERE