Baada ya kuwasili nchini Tunisia jana, moja kwa moja kikosi cha Yanga kilianza maandalizi yake katika mji wa Sousse kuelekea mchezo dhidi ya Club Africain ambao utapigwa Jumatano, Novemba 09
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri, ari iko juu kuelekea mchezo huo ambao Yanga inahitaji kushinda au kupata matokeo ya sare ya mabao ili kutinga makundi
Harrison amesema wameamua kuweka kambi nje ya Mji wa Tunis ili kuwapa utulivu wachezaji na kuzingatia program za mazoezi
Club Africain inatokea katika mji wa Tunis, ni wazi kama Yanga ingeweka kambi katika mji huo wangeweza kukumbana na matukio mengi ya nje ya uwanja
AKizungumzia hali ya hewa, Harrison amesema kuna baridi kali lakini kwa kuwa wamefika nchini humo mapema, wataweza kuzoea hali ya hewa
Yanga itarudi Tunis Jumanne na watafanya mazoezi yao ya mwisho siku hiyo tayari kuwakabili Club Africain