Msafara wa kikosi cha Yanga unatarajiwa kuondoka leo nchini Tanzania kuelekea Tunisia wakipitia Dubai ambapo wanatarajiwa kuwasili Tunisia siku ya Jumamosi majira ya mchana
Yanga inatarajiwa kuweka kambi ya siku chache huko Tunisia kabla ya mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ambao utapigwa Novemba 09
Yanga imedhamiria kwenda kusaka matokeo ya ushindi huko Tunisia ili kutinga hatua ya makundi
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ndiye mwenye ramani ya mpango mkakati wa kutinga makundi huko kwao Tunisia
Kuwa na kocha Nabi ambaye ni raia wa Tunisia ni faida kubwa kuelekea mchezo huo kwani anaweza kuisaida Yanga kukwepa mbinu chafu za wenyeji wao Club Africain
Kwenda mapema Tunisia ni sehemu ya mkakati wake, kwani timu itakuwa na siku nne za maandalizi na kuzoea hali ya hewa
Mchezo wa Novemba 09 utakuwa kama fainali, Yanga inakwenda kucheza fainali hiyo