Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama klabu ya Yanga Simon Patrick amesema sio mashabiki tu walioumizwa na matokeo ya mchezo dhidi ya Club Africain bali hata wao viongozi wameumia sana
Simon amesema uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said wamefanya kila kitu kwa ajili ya timu iweze kupata matokeo na kuwafurahisha mashabiki wake lakini haikuwezekana
Amesema uongozi umepokea maoni, mapendekezo na ushauri kutoka kwa kila mmoja na wameahidi kufanyia kazi
"Wanachokifanya mashabiki wa Yanga kutoa ya moyoni ni sahihi kabisa kwani ndiyo haki kubwa waliyonayo. Kama Viongozi tumeumizwa sana na matokeo ya jana ukizingatia tumefanya kila kitu kiutendaji kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki wetu lakini mambo hayakwenda kama tulivyotarajia"
"Uongozi huu ni sikivu sana, umepokea na unaendelea kupokea maoni na ushauri wenu, tutayachakata na kuyafanyia kazi. Rais wetu na Kamati ya Utendaji wamejitahidi kuhakikisha Yanga ina kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya timu, lakini matokeo yamekua kinyume na matarajio"
"Nawaomba tuendelee kuisapoti timu yetu kwenye mchezo wa marudiano Tunisia, mambo mengine tuwaachie viongozi mliowapa dhamana, wana malengo makubwa sana na timu," ameandika Simon kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii