Jioni ya leo kikosi cha Yanga kinatupa karata muhimu katika michuano ya kombe la Shirikisho kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi
Saa 10 jioni Yanga itakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kumenyana na Club Africain katika mchezo ambao Wananchi wanahitaji ushindi
Ndio! Yanga inahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi
Mchezo hautakuwa mwepesi lakini Yanga ina kila sababu ya kushinda mchezo huo
Wachezaji wanapaswa kupambana kwa jasho na damu ili kuhakikisha wanairejesha heshima ya Yanga kwenye michuano ya CAF
Yanga imedhihirisha ufalme wake kwenye soka la ndani ikiwa imecheza mechi 45 mfululizo pasipo kupoteza, ni ngumu kuamini kama kikosi hiki hakiwezi kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho
Mshambuliaji kinara wa Yanga Fiston Mayele amewahakikishia Wananchi leo ni siku yao ya kufurahi akiwataka wajitokeze kwa wingi uwanjani kuwashangilia
Wananchi wamechoka kuwa wasindikizaji kwenye michuano ya Kimataifa, leo ndio siku ya kufungua ukurasa mpya katika michuano hiyo
TUKUTANE KWA MKAPA...!