Yanga imechagua muda sahihi kuwakabili Club Africain kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho
Mtanange utapigwa kuanzia saa 10 jioni ambao ni muda sahihi kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenda kuishangilia timu yao
Lakini pia ni muda sahihi kucheza dhidi ya timu kutoka Afrika ya Kaskazini
Joto la Dar es salaam na jua la saa 10 inaweza kuwa silaha muhimu katika mkakati wa kushinda mchezo huo
Mara nyingi timu za Mataifa ya Kaskazini huchagua mechi zao kupigwa usiku sana kutokana na hali yao ya hewa ya baridi
Ni bahati mbaya CAF wameonda ratiba ya mechi za saa tisa mchana, pengine huu muda ungefaa zaidi
Wananchi wanapaswa kununua tiketi kwa wingi ili kuhakikisha uwanja wa Benjamin Mkapa unafurika ili wakose pumzi....!