Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi hana kazi kubwa ya kufanya katika maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain
Mchezo huo utapigwa kesho Jumatano, Novemba 02 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, wachezaji wa Yanga waliumia sana kwani wanaamini walistahili kutinga makundi ya michuano hiyo
Hii ni nafasi nyingine kwao kuhakikisha wanapata matokeo yatakayowapeleka makundi ya Shirikisho
Wachezaji wenyewe kwa wenyewe wanahamasishana na wote wakiwa na lengo moja tu, kushinda mchezo dhidi ya Club Africain
Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi kutokana na umuhimu wake lakini kwa Yanga hakuna matokeo muhimu uwanja wa nyumbani zaidi ushindi
Yanga haijawahi kuwa na matatizo makubwa katika mechi wanazocheza ugenini, walidhihirisha hilo dhidi ya Al Hilal licha ya kufungwa bao 1-0
Hivyo ushindi wa nyumbani utawaweka katika nafasi nzuri ya kutinga makundi