Kiwango bora alichoonyesha katika mechi mbili zilizopita dhidi ya KMC na Geita Gold, kinampa nafasi Ibrahim Bacca kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain
Bacca ameonyesha utayari wa kutumika katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo na huenda kocha Nasreddine Nabi akampa nafasi
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema Bacca amewaongezea wigo katika machaguo ya wachezaji wa kuwatumia kwenye safu ya ulinzi
"Bacca amecheza vizuri mechi zilizopita hili jambo jema kwake na timu kwa ujumla kwani ametuongezea ubora kwenye safu ya ulinzi," alisema
Baada ya nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto kukabiliwa na matatizo ya kifamilia, Bacca anaonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuanza mbele yake baada ya kuonyesha ubora katika mechi alizopewa nafasi
Dickson Job na Bacca wameonyesha 'ukatili' dhidi ya washambuliaji wa timu pinzani licha ya maumbile ya miili yao kuwa madogo