Nahodha wa Yanga Bakari Nondo 'Mwamnyeto' sio miongoni mwa wachezaji waliosafiri mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa leo Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema Mwamnyeto hakujumuishwa katika msafara baada ya kupata matatizo ya kifamilia
Aidha Kaze amesema kiungo Khalid Aucho ambaye amemaliza adhabu ya kadi tatu za njano, atakosa mchezo dhidi ya Geita Gold akiendelea kupona majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya Simba

Wachezaji Djuma Shaban, Joyce Lomalisa na Fiston Mayele nao walikuwa na changamoto za majeraha, wamejumishwa kikosini na jana walishiriki mazoezi ya mwisho yaliyofanyika uwanja wa CCM Kirumba
Habari njema kwa Wananchi ni kurejea kikosini kwa Bernard Morrison ambaye amemaliza adhabu ya kukosa mechi tatu. Morrison yuko fit kuwakabili Geita Gold leo