Ratiba ngumu lakini tunapambana - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Oct 2022
Ratiba ngumu lakini tunapambana - Kaze

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema mchezo dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba, utakuwa wa nne katika siku 10 kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara 

Kaze amesema ni ratiba ngumu wanayokabiliana nayo lakini watapambana kuhakikisha wanatimiza malengo ambayo ni kushinda mchezo huo

"Mechi dhidi ya Geita Gold itakuwa ya nne tunacheza ndani siku kumi, hakuna mwili wa binadamu unaweza kuhimili hili na ndio maana mnaona baadhi ya michezo tunafanya mabadiliko lakini tunahakikisha hayaathiri utendaji na malengo kwenye kipindi hiki kigumu," alisema Kaze

Aidha akizungumzia mchezo huo, Kaze amesema hautakuwa mchezo rahisi kwani Geita Gold wameimarika lakini pia wana kumbukumbu ya ugumu wa mechi walizocheza nao msimu uliopita

"Timu ya Geita imeimarika sana na toka mwaka jana Geita haijawahi kuwa mechi rahisi. Tunajua tunakwenda kwenye mechi ngumu na wana Wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa ligi lakini tumejiandaa vizuri na tutaingia kwenye mchezo wa kesho kwa nguvu kubwa"

Kaze amesisitiza Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na malengo yake na si kufikiria takwimu walizoweka

"Tunaingia kwenye kila mchezo kwa malengo hatuingii kwenye mechi kwa sababu ya kuendeleza takwimu ya kucheza bila kupoteza maana unaweza usipoteze mechi lakini ukakosa kutimiza malengo ya Klabu. Kwetu sisi kitu kikubwa na malengo yetu ni kupata alama tatu kwenye kila mchezo"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’