Katika mchezo dhidi ya KMC, mashabiki walioshuhudia mchezo huo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, ilipofika dakika ya 43 walisimama kwa dakika moja ikiwa ni heshima kwa Kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi kwa kuiwezesha Yanga kucheza mechi 43 pasipo kupoteza
Yanga itaendeleza utaratibu huo katika mchezo dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Sasa ni mechi 44, hivyo mashabiki katika uwanja wa CCM Kirumba watasimama itakapofika dakika ya 44 kumpigia makofi Nabi na benchi lake la ufundi
ADVERTISE HERE