Winga Bernard Morrison ni miongoni mwa wachezaji waliojumuishwa kwenye kikosi cha Yanga ambacho kimetua jijini Mwanza kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold
Yanga imethibitisha kuwa Morrison amemaliza adhabu ya kufungiwa mechi tatu na sasa yuko huru, ataanza na Geita Gold
Adhabu ya Morrison imemalizika baada ya kukosa mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba na KMC
Aidha kiungo Khalid Aucho nae amerejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kadi tatu za njano. Alikosa mchezo dhidi ya KMC
Nyota wengine Fiston Mayele, Kibwana Shomari na Djuma Shaban ambao walipumzishwa katika mchezo dhidi ya KMC, wote wako tayari kuikabili Geita Gold siku ya kesho Jumamosi
ADVERTISE HERE