Kikosi cha Yanga kimewasili jijini Mwanza kuelekea mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba
Yanga iliondoka Dar Alfajiri ya leo ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 ambapo miongoni mwa wachezaji hao ni winga Bernard Morrison aliyemaliza adhabu ya kufungiwa mechi tatu
Wachezaji waliosafiri ni Djigui Diarra, Erick Johola, Shomari Kibwana, Joyce Lomalisa, Shabani Djuma, Yanick Bangala, Ibrahim Bacca, Dickson Job na Gael Bigirimana
Wengine ni Zawadi Mauya, Abubakar Salum, Jesus Moloko, Farid Mussa, Dickson Ambundo, Benard Morrison, Dennis Nkane, Feisal Salum, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Stephane Aziz KI na Tuisila Kisinda.





ADVERTISE HERE