Msimu huu Feisal Salum sio tu anaweza kuwa mchezaji bora wa msimu, bali haitashangaza akiwania kiatu cha dhahabu pia
Bao alilofunga jana katika mchezo dhidi ya KMC ni la nne kwake msimu huu, ukiwa ndio kwanza mchezo wa saba
Yuko nyuma kwa bao moja tu dhidi ya Reliants Lusajo wa Namungo Fc aliyefunga mabao matano
Feisal aliibuka mchezaji bora wa ligi kwa mwezi Septemba na kama atafanya vizuri katika mchezo unaofuata dhidi ya Geita Gold huenda akawania tena tuzo hiyo
Mabao anayofunga yana thamani kubwa sana kwa Yanga rejea mabao yake aliyofunga katika michezo dhidi ya Ruvu Shooting na Azam Fc
Feisal huenda akaumaliza mapema sana mjadala wa nani kiungo bora katika ligi kuu ya NBC
ADVERTISE HERE