Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo amefanya mabadiliko katika kikosi chake kinachoikabili KMC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC unaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Djuma Shaban amekosekana upande wa kulia nafasi yake ikichukuliwa na Dickson Job
Farid Mussa nae ameanza safu ya ulinzi upande wa kushoto wakati Ibrahim Bacca akianza na Mwanyeto katika ulinzi wa kati
Heritier Makambo leo anaongoza safu ya ushambuliaji wakati Ambundo akianza winga wa kushoto na Kisinda kulia
Khalid Aucho anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano wakati Mayele akikosekana kabisa katika mchezo wa leo

ADVERTISE HERE