Majira ya saa moja usiku leo Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili KMC ikiwa ni mechi ya ligi kuu ya NBC
Katika mchezo huo, Yanga itaendelea kumkosa winga Bernard Morrison anayetumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu
Utakuwa mchezo wa pili Morrison kukosekana baada ya mchezo dhidi ya Simba
Mshambuliaji Chrispine Ngushi yeye amerejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani wiki nane
Kwa ujumla, Kocha Nasreddine Nabi ataingia kwenye mchezo huo akiwa na nyota wake wote muhimu katika kuzisaka alama zote tatu
ADVERTISE HERE