Yanga kwenda Shelisheli kesho, Lwandamina atahadharisha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2018
Yanga kwenda Shelisheli kesho, Lwandamina atahadharisha
Kikosi cha wachezaji 20 wa Yanga kitaondoka nchini kesho Jumapilia kuelekea Shelisheli kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya St Louis huko kocha George Lwandamina, akisema wanaenda nchini humo kwa tahadhari kubwa.

Akizungumza baada ya mazoezi jana jioni, Lwandamina, alisema kuwa ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam utawafanya kuwa makini kwenye mchezo huo wamarudiano kwa kuwa bado hawajajihakikishia tiketi ya kusonga mbele.

"Bado tuna kazi ya kufanya, tutaingia uwanjani kwa tahadhari kujaribu kutafuta ushindi, wachezaji wapo katika hali nzuri na wanafahamu nini cha kufanya."

Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote kuweza kusonga mbele kuingia hatua ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za vilabu Afrika.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Februari 10 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga iliibuka na ushindi huo wa bao 1-0, shukrani kwa Juma Mahadhi aliyefunga bao hilo pekee.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
56m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’