Tetesi zimekuwa nyingi kuhusu kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi na hatma yake na mabingwa hao wa Tanzania
Wakati mwingine tetesi hizi zinaanzishwa kwa lengo la kuvuruga tu pale penye utulivu
Huu ni mtego mwingine ambao Wananchi hawapaswi kuingia kwa maslahi mapana ya klabu yao
Nabi amerejesha heshima ya Yanga ambayo ilipotea misimu minne iliyopita
Chini yake msimu uliopita Yanga ilitwaa mataji yote ya ndani pasipo kupoteza mchezo na wameendeleza rekodi hiyo msimu huu mpaka sasa wakiwa wamecheza mechi 43 za ligi pasipo kupoteza
Kwa mafanikio hayo, sio rahisi viongozi wa Yanga kumuondoa Nabi, ukweli ni kwamba Nabi ameiheshimisha Yanga
Presha ni kubwa baada ya Yanga kushindwa kutinga makundi ya ligi ya mabingwa lakini bado iko nafasi nyingine kwenye kombe la Shirikisho
Kama Yanga italeta kocha mpya sasa maana yake ni kuwa atahitaji muda kutengeneza kikosi chake
Yanga haina muda huo kuelekea mchezo dhidi ya Club Africain Novemba 02