Micho alikuwepo uwanjani kuwashuhudia Wananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Oct 2022
Micho alikuwepo uwanjani kuwashuhudia Wananchi

Jana katika mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Uganda Milutin Micho alikuwepo uwanjani kushuhudia mtanange huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Akizungumza na wanahabari baada ya mchezo huo, Micho aliyewahi kuwa Kocha wa Yanga, alibainisha kuwa kilichomleta ni kuangalia mchezo hasa kumuona kiungo Mganda Khalid Aucho

Micho alibainisha kuwa bado mahaba yake na Yanga hayajaisha na alifurahishwa na mtanange huo akimtaja Stephane Aziz Ki kuwa mchezaji aliyemvutia zaidi

"Yanga ni familia yangu, nimekuja kuitazama na nimefurahushwa na mchezo wa leo. Nimevutiwa na Aziz Ki ni mchezaji mzuri sana sio kwa sababu amefunga lakini toka dakika ya kwanza mechi inaanza alionesha ana uwezo mkubwa na nguvu nyingi. Hata Aucho (Khalid) amecheza vizuri, yeye anaonekana kuwa mhimili wa Yanga, amekuwa na kiwango kizuri" alisema Micho

Kumekuwa na tetesi nyingi juu ya ujio wa Micho nchini, hata hivyo mwenyewe amesisitiza hakuna jambo jingine nje ya kushuhudia mchezo huo hasa kumuona Aucho ambaye ni mmoja wa wachezaji wake katika timu ya Taifa ya Uganda

"Nilikuja kutazama mechi na si kwa mipango mingine. Bado nina mkataba na timu ya taifa ya Uganda na sijafanya mazungumzo ya timu yoyote zaidi ya kusalimiana na viongozi wa Yanga maana ni wadau wenzangu katika soka" 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’