Tangu GSM walipoingia kuidhamini Yanga, mabingwa hao wa Tanzania hawajawahi kupoteza mchezo wowote wa ligi kuu dhidi ya Simba
Mara ya mwisho Yanga kufungwa na Simba kwenye ligi ni Februari 2019, wakati huo Yanga ikinolewa na Kocha Mwinyi Zahera
Baada ya msimu huo kumalizika ndipo Kubwa Kuliko ikaandaliwa na GSM kuichangia Yanga Tsh Milioni 300
Huo ndio ukawa mwanzo wa Yanga mpya ambayo msimu mmoja baadae ikafanikiwa kutwaa mataji yote ya ndani
Ni hivi; Yanga na Simba zimekutana mara sita kwenye ligi tangu ujio wa GSM, Yanga imeshinda mechi mbili na nne zikamalizika kwa matokeo ya sare
Kesho Yanga na Simba zinakutana tena katika mchezo wa ligi kuu ambao Yanga ni wenyeji
ADVERTISE HERE