Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya St louis.
Yanga itaikabili St Louis nchini Sychelles Jumatano ya February 21, 2018 na inatarajiwa kuondoka keshokutwa Jumapili.
Bado Amissi Tambwe, Abdallah Shaibu, Donald Ngoma na Yohana Nkomola wameendelea kukosekana kwenye kikosi cha Yanga kutokana na majeruhi.
Huenda wanne hao wasiwemo kwenye msafara wa watu 30 (wachezaji 20 na viongozi 10) wanaotarajiwa kusafiri keshokutwa.
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema Yanga imejipanga kuhakikisha inapata ushindi kwenye mchezo ili kuweza kusonga mbele raundi ya kwanza.
Iwapo itafanikiwa kufuzu Yanga huenda ikachuana na Rollers ya Botswana iliyoilaza El Mareikh ya Sudan kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza.

ADVERTISE HERE