Wachezaji 'wanautaka' mchezo dhidi ya Simba - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Oct 2022
Wachezaji 'wanautaka' mchezo dhidi ya Simba - Kamwe

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji wameumizwa sana na matokeo ya kushindwa kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa huku wakifahamu kwa kiasi gani wamewaumiza mashabiki wao

Kamwe amesema wachezaji wa Yanga wanahitaji nafasi nyingine kuwaonyesha mashabiki wao kuwa bado wako imara na kuwa kukosa kufuzu makundi ligi ya mabingwa walikosa bahati tu

Wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya Simba kuongeza morali kuelekea mchezo wa Shirikisho dhidi ya Club Africain

"Siku tuliporejea kutoka Sudan mchezaji wa kwanza kuzungumza na wanahabari alikuwa Fiston Mayele. Kuonyesha ni kwa kiasi gani wamefadhaishwa na matokeo waliyopata"

"Ukiwaangalia nyuso zao utaona machungu na hasira walizonazo, wanahitaji nafasi nyingine kuwaonyesha mashabiki kwa vitendo kuwa kilichotokea ni bahati mbaya"

"Tunashukuru Bodi ya Ligi kwa kutupangia mchezo dhidi ya Simba baada ya mechi ya Al Hilal kwani wachezaji wameapa kutumia mchezo huo kuwaomba radhi mashabiki kwa vitendo"

"Tunachowaambia mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili, kuna jambo kubwa tumewaandalia. Watani zetu tunawaambia waje uwanjani si wanasema timu yetu mbovu! Waje uwanjani tuonyeshane na sio kufanya propaganda 'kudogosha' dabi baada ya kuona hawawezi kutufunga," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’